Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka akikabidhiwa zawadi ya fulana na Mkurugenzi wa uhusiano na sheria wa TBL, Steven Kilindo yenye ujumbe wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani baada ya mkuu huyo kuzindua rasmi upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha. katikati ni Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga na kulia ni kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Willie Mwamasika
Sunday, 28 September 2014
PRESIDENT KIKWETE VISITS CNN STUDIOS IN NEW YORK ON SEPTEMBER 26, 2014
Wednesday, 28 May 2014
WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI AFANYA ZIARA WILAYANI MVOMERO
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akipata maelezo ya jiwe la alama ya mpaka (beacon) unaotenganisha vijiji vya Dihombo na Mkindo wilayani Mvomero kabla ya kukabidhi hatimiliki za kimila jana. Hatua ya kutolewa hati ni baada ya kazi ya kupanga matumizi ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji na hatimaye kumaliza mgogoro uliokuwepo awali. Anayetoa maelezo ni Mpima Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Bw. Musa Stephen.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akishiriki kusoma ramani za mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji cha Lukenge Wilayani Mvomero uliopangwa na wanakijiji wenyewe.
Sunday, 20 April 2014
Monday, 10 March 2014
Wakazi wa Morogoro mjini wapatiwa elimu ya lishe
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Anthony Mtaka(Kushoto)akiwa na wataalamu wa lishe toka USAID Tuboreshe chakula.Akishiriki kwa vitendo katika kuandaa uji wa mtoto,miezi 6 – miaka 5 kuchanganya virutubishi ,tayari kwa kumnywesha mtoto,katika kampeni za uhamasishaji na uelimishaji wa virutubishi,katika viwanja vya Shule ya msingi Mafisa A mkoani Morogoro.Kampeni hizi zimedhaminiwa na shirika la misaada la marekani USAID Tuboreshe chakula.
Mkuu wa wilaya Mvomero,Anthony Mtaka akimnywesha uji, mmoja wapo wa watoto waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa siku ya Virutubishi viwanja vya shule ya msingi Mafisa A,mkoani Morogoro. lengo la kampeni ni kuhamasisha,kuelimisha umuhimu na faida za virutubishi kwa watoto walio na umri kati ya miezi 6-miaka 5. Kampeni hizi zimefadhiliwa na Shirika La misaada la Watu wa Marekani (USAID) kupitia Mradi wa Tuboreshe Chakula.
Saturday, 1 February 2014
TANSEED INTERNATIONAL NA MIKAKATI YA KUHAMASISHA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU BORA YA MPUNGA YA TXD 306 'SARO 5' KATIKA BONDE LA WAMI-DAKAWA MVOMERO MOROGORO.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka naye akizungumza jambo katika mkutano huo, kutoka kushoto ni, Isaka Mashauri na Mkuu wa mkoa Joel Bendera.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (katikati) akidadisi jambo kwaMkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri kulia kwake wakati wa maonyesho ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5) katika shamba la mkulima wa zao la mpunga Nassibu Katoto mbele lililopo katika bonde la Wami-Dakawa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Friday, 31 January 2014
WAZIRI MKUU ATEMBELEA ENEO LA DARAJA LILILOATHIRIWA NA MAFURIKO MKOANI MOROGORO
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (kushuto ) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Mh. Anthony Mtaka wakati alipotembelea sehemu iliyoathirika kwa mafuriko,Mkoani Morogoro.
Friday, 3 January 2014
UZINDUZI RASMI WA MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2013 , KINGOLWIRA MOROGORO WAFANA
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka, Akizungumza pamoja na wakazi wa eneo la Kingolwira pamoja na wageni mbalimbali waliotoka sehemu mbalimbali Tanzania na kutoa tamko rasmi la kuzindua shindano la Maisha Plus/ Mama shujaa wa chakula 2013
DC MVOMERO AFUNGUA MKUTANO WA WASABATO TURIANI MOROGORO.
DC Mtaka akizngumza na Mkurugenzi wa Global Mission kutoka Ukraine Mchungaji Dmitry Zubbkov kulia na katikati ni Dkt Alex Magufwa baada ya mkuu huyo kumaliza kufungua mkutano Mkuu wa dini unaofanyika katika vijiji viwili vya Kialawa na Lukenge na ambapo wananchi wa maeneo ya jirani mkoani hapa, kulia ni mchungaji wa mtaa wa kanisa hilo, Leonard Mbushi na katikati ni mkuu wa wilaya mstaafu wa Kwimba mkoani Mwanza, Reuben Matongo.
Sehemu ya watoto katika kijiji cha Kialawa na waumini wa kanisa hilo wakifuatia matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi huo.
Kwaya ya kanisa hilo la Kialawa wakitumbuiza kwa nyimbo za mapambio.
Mkurugenzi wa Global Mission kutoka Ukraine Mchungaji Dmitry Zubbkov kulia akifafanuliwa jambo kutoka kiswahili na KiUkraine na Dkt Alex Magufwaambaye ni mwenyeji wake wakati mkuu wa wilaya ya Mvomero akifungua mkutano huo wa dini.
MKUU WA WILAYA YA MVOMERO MHE ANTHONY MTAKA AKIAPA MBELA YA MKUU WA MKOA WA MOROGORO MHE JOEL BENDERA
MHE ANTHONY MTAKA AKIKABIDHIWA ZAWADI YA MAUA NA MAMA YAKE MZAZI KATIKA HAFLA HIYO
Subscribe to:
Posts (Atom)