MKUU WA WILAYA


WASHINDI WA TUZO ZA EXCEL WITH GRAND MATL MKOA WA MOROGORO WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO

 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Mh. Anthony Mtaka (katikati) ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye Sherehe za utoaji wa Zawadi kwa Washindi wa Tuzo za Excel With Grand Malt 2012 kwa vyuo vya Mzumbe na Sokoine vya Mkoani Morogoro,akizungumza machache kabla ya kuanza kwa zoezi la utoaji wa zawadi hizo kwa washindi mbali mbali walioshiriki kikamilifu kwenye shindano hilo.Sherehe hizo zimefanyika jioni hii kwenye viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mkoani Morogoro.Kulia ni Meneja kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Tuzo hizo,Consolata Adam na Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mzunge,Prof. Faustin Kamuzola.
 Meneja kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Tuzo Excel With Grand Malt 2012,Consolata Adam akitoa shukrani zake kwa Vyuo vyote vilivyoweza kushiriki katika Mashindano hayo muda mfupi kabla ya kuanza kwa zoezi la utoaji wa zawadi hizo leo.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mzunge,Prof. Faustin Kamuzola (kushoto) akizungumza wakati wa sherehe hizo.
 Washindi mbali mbali wa tuzo za Excel With Grand Malt kutoka Vyuo vya Mzumbe na Sokoine wakiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Vyuo hivyo,Wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, wakionyesha fedha zao walizoshinda mara baada kukabidhiwa jioni ya leo kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Mzumbe.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Mh. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) akikabidhi Cheti cha Shukrani kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mzumbe,Prof. Faustin Kamuzola (kulia) ikiwa ni heshima ya kuruhusu Chuo hicho kushiriki kwenye Mashindano hayo.Kushoto ni Meneja kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Mh. Anthony Mtaka (wa pili kulia) akikabidhi fedha kwa washindi mbali mbali wa Tuzo za Excel With Grand Malt 2012 jioni ya leo kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Mzumbe,Mkoani Morogoro. 
 Mdau Victor Ndunguru (kushoto) akiwapatia zawadi za mabegi washindi wa bahati nasibu ndogo iliyochezeshwa hapo.
 Mchezo wa kuzungusha ringi kiunoni.
 Kuvuta kamba kati ya Chuo cha Mzumbe na Sokoine,ambapo chuo cha Mzumbe wameibuka kidedea.
 Soka ndio ilikuwa mpango mzima,hapa ni Bambi kwa Bambi........
 Kazi ya Beki huwa haina sifa kwa kawaida,hapa jamaa ameamua kula zote ili kuokoa mpira usiende lakoni kwake.
 kitu na box.........
 kupimana msuli kama kawa,katika mtanange huu uliowakutanisha Wanafunzi wa Vyuo vya Mzumbe na Sokoine,uliweza kuwapa ushindi mnono timu ya Sokoine kwa mabao 6-2.
 hapiti mtu hapaaa.....
 kata kiu na Grand Malt.
 Prof Jay ndie alieweza kusindikiza Shereha za utoaji wa Tuzo hizo kwa mapini yake makali makali.

No comments:

Post a Comment