Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Anthony Mtaka(Kushoto)akiwa na wataalamu wa lishe toka USAID Tuboreshe chakula.Akishiriki kwa vitendo katika kuandaa uji wa mtoto,miezi 6 – miaka 5 kuchanganya virutubishi ,tayari kwa kumnywesha mtoto,katika kampeni za uhamasishaji na uelimishaji wa virutubishi,katika viwanja vya Shule ya msingi Mafisa A mkoani Morogoro.Kampeni hizi zimedhaminiwa na shirika la misaada la marekani USAID Tuboreshe chakula.
Mkuu wa wilaya Mvomero,Anthony Mtaka akimnywesha uji, mmoja wapo wa watoto waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa siku ya Virutubishi viwanja vya shule ya msingi Mafisa A,mkoani Morogoro. lengo la kampeni ni kuhamasisha,kuelimisha umuhimu na faida za virutubishi kwa watoto walio na umri kati ya miezi 6-miaka 5. Kampeni hizi zimefadhiliwa na Shirika La misaada la Watu wa Marekani (USAID) kupitia Mradi wa Tuboreshe Chakula.
Mkuu wa wilaya Mvomero,Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Mshauri wa Rais mambo ya lishe,Dr .W. Lorri (Kulia).Katika siku ya sherehe za uhamasishaji wa virutubishi kwa watoto umri wa miezi 6-miaka 5 Mkoani Morogoro. Kampeni hii iko chini ya mradi wa Tuboreshe Chakula unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani USAID.
Mtaalamu wa lishe Nuria.K.Majaliwa akitoa mafunzo juu ya virutubishi na umuhimu wa unga lishe,kwa aliyekua mgeni rasmi Bw Anthony Mtaka Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,(Kulia) pembeni yake ni Mkurugenzi Mkaazi wa USAID Tuboreshe Chakula,Rebecca Savoure katika sherehe za uzinduzi wa siku ya virutubishi.Lengo ikiwa ni kusisitiza na kuelimisha faida na umuhimu wa virutubishi kwa watoto umri wa miezi 6 – miaka 5,ikiwa ni mkakati wa Serikali ya Tanzania,ikishirikiana na USAID tuboreshe chakula,Kupunguza utapiamlo nchini.
No comments:
Post a Comment