Sunday 28 September 2014

TBL YAFANIKISHA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA WIKI YA NENDA KWA USALAMA

 Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka akikabidhiwa zawadi ya fulana  na Mkurugenzi wa uhusiano na sheria wa TBL, Steven Kilindo yenye ujumbe wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani baada ya mkuu huyo kuzindua rasmi upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha. katikati ni Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga na kulia ni kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Willie Mwamasika

PRESIDENT KIKWETE VISITS CNN STUDIOS IN NEW YORK ON SEPTEMBER 26, 2014

1

President Jakaya Mrisho Kikwete chats with  Cable News Network (CNN) ‘s Richard Quest and Maggie Lake when he visited  CNN Studios at the  Time Warner Cente in New York.  

Wednesday 28 May 2014

WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI AFANYA ZIARA WILAYANI MVOMERO














































Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akipata maelezo ya jiwe la alama ya mpaka (beacon) unaotenganisha vijiji vya Dihombo na Mkindo wilayani Mvomero kabla ya kukabidhi hatimiliki za kimila jana. Hatua ya kutolewa hati ni baada ya kazi ya kupanga matumizi ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji na hatimaye kumaliza mgogoro uliokuwepo awali. Anayetoa maelezo ni Mpima Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Bw. Musa Stephen. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anna Tibaijuka akishiriki kusoma ramani za mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji cha Lukenge Wilayani Mvomero uliopangwa na wanakijiji wenyewe. 

Monday 10 March 2014

Wakazi wa Morogoro mjini wapatiwa elimu ya lishe

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Anthony Mtaka(Kushoto)akiwa na wataalamu wa lishe toka USAID Tuboreshe chakula.Akishiriki kwa vitendo katika kuandaa uji wa mtoto,miezi 6 – miaka 5 kuchanganya virutubishi ,tayari kwa kumnywesha mtoto,katika kampeni za uhamasishaji na uelimishaji wa virutubishi,katika viwanja vya Shule ya msingi Mafisa A mkoani Morogoro.Kampeni hizi zimedhaminiwa na shirika la misaada la marekani USAID Tuboreshe chakula.
Mkuu wa wilaya Mvomero,Anthony Mtaka akimnywesha uji, mmoja wapo wa watoto waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa siku ya Virutubishi viwanja vya shule ya msingi Mafisa A,mkoani Morogoro. lengo la kampeni ni kuhamasisha,kuelimisha umuhimu na faida za virutubishi kwa watoto walio na umri kati ya miezi 6-miaka 5. Kampeni hizi zimefadhiliwa na Shirika La misaada la Watu wa Marekani (USAID) kupitia Mradi wa Tuboreshe Chakula.

Saturday 1 February 2014

TANSEED INTERNATIONAL NA MIKAKATI YA KUHAMASISHA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU BORA YA MPUNGA YA TXD 306 'SARO 5' KATIKA BONDE LA WAMI-DAKAWA MVOMERO MOROGORO.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka naye akizungumza jambo katika mkutano huo, kutoka kushoto ni, Isaka Mashauri na Mkuu wa mkoa Joel Bendera. 
 
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (katikati) akidadisi jambo kwaMkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri kulia kwake wakati wa maonyesho ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5) katika shamba la mkulima wa zao la mpunga Nassibu Katoto mbele lililopo katika bonde la Wami-Dakawa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Friday 31 January 2014

WAZIRI MKUU ATEMBELEA ENEO LA DARAJA LILILOATHIRIWA NA MAFURIKO MKOANI MOROGORO

Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (kushuto )  pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Mh. Anthony Mtaka wakati alipotembelea sehemu iliyoathirika kwa mafuriko,Mkoani Morogoro.